Habari wapendwa nipo pamoja nanyi mpaka kieleweke leo tuzungumzie japo kwa uchache maelezo ya kufanya Root kwenye simu zetu za android
kabla ya kuanza kuroot simu yako kutabatilisha warranty na muuzaji wako aliyekuuzia , pi root at your own risk i will not be hold responsible for any negative outcomes
ANDROID ROOTING NI NINI?
Ni mchakato
wa kuruhusu watumiaji wa smartphones, Tablet na vifaa vingine
vinavyotumia Oparetion sysetm ya android kupata uwezo kukiendesha kifaa
au simu ya android katika kiwango cha hali ya juu
Rooting mara nyingi hutumika kwa lengo la kuondo overcome limitations ambazo zimewekwa na watengenezaji wa vifaa vya android
FAIDA ZA KU-ROOT
Rooting ina
faida nyingi kama vile kubadiri ROOM, Kuinstall system installed app
ku install apps ambazo zinahitaji root access kama vile TITANIUM BACK
UP

JINSI YA KUROOT
Ku root
android devices kunatofautiana kati ya simu na simu , hapa nitakupatia
njia za ku root baadhi ya simu na baadhi ya vision za android
1) Huawei Idoes U8150
- wengi wetu tuna miliki simu aina hii HUAWEI IDOES U8150 simu ya aina hii ni rahisi sana fuata utaratibu huu
- download app inayoitwa z4root download z4root hapa http://search.4shared.com/q/1/z4root.apk
- kisha install z4root
- fungua z4root
- kisha bonyeza sehemu iliyoandikwa PERMANENT ROOT
Natumai tutakuwa tumepata mwanga japo kwa uchache kuhusu Rooting kwenye simu zetu za android
AU;
Njia rahisi kabisa ya kuroot smartphone ya Android OS.
Kipindi cha nyuma nilishawahi kuelezea katika blogu hii maana ya rooting.
Katika operating system ya Android, rooting ni mchakato wa kufungua
mfumo(system) wa Android ili kuweza kupata uwezo zaidi wa kuitawala
smartphone yako. Operating system huwa na makabrasha(files and folders)
ambayo huwezi pata uwezo wa kuyafanya chochote mpaka utapofanya mchakato
wa rooting.
Unaporoot smartphone ya Android tunasema kwamba umepata "system
privileges" ikimaanisha kwamba una vipaumbele vya kuweza kuitawala
operating system ya simu yako. Hii itakuwezesha kufuta apps zilizopo
katika system, kuzifanya apps unazodownload katika playstore kuwa apps
za system(changing application softwares into system softwares),
kubadili maandishi(fonts), kuweka operating systems zisizo rasmi(custom
roms) na mengineyo mengi.
Kuna njia ambazo hutumika ili kuwezesha rooting kukamilika. Unaweza
tumia programu za kompyuta au programu(apps) za Android, inategemea na
njia unayochagua kutumia. Kuna baadhi ya njia ambazo hupunguza ugumu wa
mchakato huu. Nitaelezea njia moja ambayo kwa sasa ni rahisi sana na
inakubali katika smartphone za aina nyingi mno kuanzia Huawei mpaka HTC.
Njia hii hutumia programu(app) ambayo utaidownload na kuinstall katika
smartphone yako, app inafahamika kama Towelroot. Kwa kutumia app hii,
rooting ni mchakato wa dakika moja tu!. Nitaeleza hatua za mchakato
huu.
1. Katika smartphone yako ya Android ingia katika internet browser uliyonayo na kisha tembelea address hii: http://towelroot.com au unaweza ingia moja kwa moja kupitia hapa. Kisha bonyeza alama ya lambda ili kuweza kudownload file la Towelroot.
![]() |
Bonyeza lambda ili kuweza download towelroot.apk |
2. Baada ya kukamilisha kudownload towelroot.apk, ingia katika
settings za smartphone yako na kisha nenda katika security. Ndani ya
security tafuta mahala palipoandikwa "unknown sources", hakikisha sehemu hii ipo activated.
![]() |
Hutaweza install "towelroot.apk" kama unknown sources ipo deactivated. |
3. Baada ya kukamilisha hatua ya pili, rudi katika internet browser yako kisha install "towelroot.apk".
4. Baada ya kufanya installation, fungua app ya towelroot katika menu yako. Baada ya kufunguka, bonyeza palipoandikwa "make it ra1n" .
![]() |
Hakikisha simu yako ina mtandao(internet) wakati unafanya hatua hii. |
5. Kama rooting imekubali katika smartphone, utatokea ujumbe
unaoonekana hapo chini katika screenshot. Kama smartphone yako itakataa
kuwa rooted kwa hii app itajizima na kujiwasha, hakutakuwa na madhara
yoyote.
6. Baada ya hapo, utahitaji kudownload app kwa ajili ya
kupata ruhusa za kuingia katika system ya Android. App hii inaitwa Super
User(SuperSU). Utaipata Playstore, ingia Playstore na kisha tafuta
"SuperSU" halafu install.
7. Baada ya installation, fungua SuperSU na kisha update kwa kuchagua continue, updte kwa kutumia "normal".
8. Baada ya ujumbe unaoonekana hapo chini kukamilika kwa
kusema "installation complete". Hapo utakuwa tayari umesharoot
smartphone yako ya Android, tayari kuitumia kama Super User. Utahitajika
kureboot na baada ya hapo unakuwa umekamilisha mchakato mzima.
Ili kuangalia kama mchakato wa kuroot umefanikiwa kabisa, unaweza kutumia app ambayo inafanya kazi ya kuangalia root access kwenye simu yako, chagua langu huwa ni hii hapa ambayo inapatikana PlayStore "Root Checker". Lakini zipo nyingi sana playstore, chaguo ni lako
No comments:
Post a Comment